Katika wilaya ya Chemba, Kata ya Ovada, kijiji cha Kilimba kumetokea mauaji ya watu wawili. Mauaji hayo yalitokea baada ya kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Jumanne kumkatakata na nyengo mtu anayesadikiwa kuwa ni shemeji yake aliyetambulika kwa jina la Kamili mpaka kumuua. Baada ya kufanyatukio hilo Jumanne alikimbilia kijiji cha Lahoda ambako alifuatwa na wananchi wenyehasira na walipo mtia mikononi mwao walimpiga sana kiasi cha kuhatarisha uhai wake. Mtuhumiwa alifanikiwa kufikishwa kituo cha polisi Kwa Mtoro ambapo alipoteza maisha. Enzi za uhai wake mtuhumiwa Alishawahi kuhukumiwa kwa kosa kama hili la mauaji na alitumikia kifungo mpaka kumaliza na alipoachiwa aliishi kwa muda kabla ya kurudia kosa lililo mgharimu kifo.
Siku yatukio mtuhumiwa ambaye ni marehemu kwa sasa alikuwa na marehemu Kamili katika nyumba mbalimbali za pombe kabla ya kurudi nyumbani kwa shemeji yake (Kamili) na kuomba nyengo kwa Dada yake na alipopewa alimkata shemeji yake kiunoni,shingoni na shavuni ndipo mrehemu Kamili alianguka na kupoteza uhai.
Hapo hapo
Mtu mmoja amechinjwa hadi kufa na mtu anayeaminika kuwa ni mganga wa jadi katika kijiji cha Chamwino ikulu wilaya ya Chamwino,mkoani Dodoma. Mganga huyo alifanyatukio hilo wakati akitoa huduma kwa mteja wake huyo, nyumbani kwa mteja wake,siku ya Jumapili majira ya saa nne asubuhi katika kijiji hicho cha Chamwino Ikulu wilaya ya Chamwino.