
Unaweza ufananisha ujenzi wa maendeleo na ujenzi wa nyumba jinsi ambavyo nyumba huunganisha chembe ndogondogo za mchanga mpaka kuwa nyumba. Maendeleo huanza na mtu mmoja,familia,koo,jamii na kuendelea mpaka ngazi ya dunia kuwa na maendeleo. Afrika kama zilavyo sehemu nyingine za duniainahitaji na inahaki ya kupata maendeleo katika nyanja mbalimbali kama vile uchumi,utamaduni,siasa na kijamii. Uwezo wa kuendelea katika nyanja hizo upo,nia ya kuendelea ipo na hii inatokana na bara lenyewe lilivyo tunukiwa mali na rasilimali za kila namna ukilinganisha na mabara mengine.
Afrika kuna madini ya kila namna ambayo mengine hayapatikani kwingine kote duniani. Afrika kuna mafuta ya kutosha. Afrika ina ardhi kubwa na yenye rutuba kuliko sehemu yoyote ulimwenguni. Afrika kuna vipaji vingi sana. Afrika kuna wasomi wengi sana. Afrika ina watu wenyenguvu za asili ukilinganisha na mabara mengine. Lakini afrika inaongoza kuwa na viongozi na watu wavivu wavivu na wazembe wenye ubinafsi,chuki na wivu kuliko sehemu nyingine yeyote duniani. Afrika ndio bara pekee duniani ambalo nchi zake zinajiendesha kwa mikopo na misaada kutoka Amerika na Uraya.
Ubinafsi.
Afrika inaongo kuwa na watu wanaojifikiria wao kwanza wengine badae. Ubinafsi ni mungu wa mwafrika. Umekithri mno mpaka ndani ya familia. Usishangae baba kumtoa mtoto wake kafara ili apate mali ukiwa ndani ya Afrika. Na hilo wala halitamuwazasha baba huyo. Swali la kujiuliza ni je mali anayoitafuta ni kwa ajiri ya nani, kama kizazi chake kateketeza? Maana kila lifanyikalo leo huwa na dhumuni la kuijenga kesho iliyobora. Hali ya ubinafsi imekua mpaka kuingia ndani ya nafsi za viongozi wa Afrika. Ndio maana habari za kung’ang’ani,kupigania au kupinduana haziishi hapa kwetu Afrika. Je, wanaonga’ng’ania na kupigania mdaraka wanawaza kuhusu nchi zao kunufaika na mitazamo yao kweli au nikutafuta furusa ya kunufaika wao na familia zao? Hata wale wachache uliosikia kuwa wameachia madara kidemokrasia basi ukichunguza walio waachia utagungua kuwa ni watoto,ndugu,marafikia au Jamaa zao wakaribu ndio waliowaachia. Hili si jambo dogo la kulonyamazia niamini mimi. Afrika ina vipaji vingi vya kutuongoza tunakokutamani. Sasa kwa nini munaifanya Afrika kuwa mali ya watu fulanifulani? Hata hapa kwetu kama Raisi huyu asingekuwa mwenyekiti wa chama chake huenda kungeanza kufanyika vikao vya siri ili kumvua uanachama kutokana na teuzi zake zinazo wapa nafasi wapinzani na si watu wa chama chake. Lakini na hawa wapinzani nao ni wapinzani kweli au ni mapandikizi ya chama tawala kwa nia ya kudhoofisha upinzani na kuendelea kuitafuna nchi kupitia chama kimoja? Kwa nini Waafrika hatuaminiani sisi kwa sisi? Hili ni tatizo linalotuondoa kwenye misingi ya weledi,nia na hamu ya kuiona Afrika moja yenye maendeleo zaidi. Badala yake tunaendekeza tamaa na tunaongozwa na ubinafsi kuelekea umasikini,njaa na ujinga.
Wivu…
Waafrika hatupendani na hatupendi kuyaona mafanikio au mambo mazuri yakiwa kwetu bila kutafuta sababu za kukosoa. Hatupendi kujifunza namna vizuri vinavyopatokana badala yake tunajifunza namna tunavyoweza kukwamisha vizuri kufika au kuwepo kwetu. Tuna wivu wa kishamba. Nakumbuka mija ya hutuba za Mwl nyerere aliwaomba wananchi wake japo watengeneze trekta la kurudi nyuma. Lakini nchi hiyo hiyo miaka hamsini uhuru wanapinga mtu kutengeneza ndege. Huyu ndio mwafrika bwana. Ukichunguza undani wa kuzuia ubunifu huo ni misaada kutoka nje ambayo wanufaika ni wachache sana. Ukitaka utajiri Afrika ungana na wanasiasa na ukitaka kufirisika afrika pingana na na siasa na mwanae. Ndivyo tunavyoishi japo tunandoto za kuujenga umoja na uchumi imara. Kalamu yangu ikuponye ewe mwafrika mwenzangu, chako changu pia ukifa utajizika mwenyewe hufikirii hilo? Talanta kila mmojaalipewa yake lakini tukizounganisha tutapata kitu chenye thamani sana. Wivu wa kipuuzi hautatufikisha mbali. Utazidi kutuimarishia ukiritimba,umaamuma,ujuha, na mabaya yote ni vyema kuachana nao. Hatushindwi tukiamua.
Chuki…
Nh! Hapa ndipo balaa lingine ndani ya Afrika. Sijui ni zimwi au ni laana hii. Waafrika wanachukiana, wanasiasa wanachukiana, wafanyakazi,watawala na watawaliwa basi ni chuki chuki chuki kwenda mbele. Ukabila,uvyama udini umetutenga kabisa waafrika. Si ulisikia mauaji ya kimbali pale Rwanda? Je, vita ya Kenya mwaka 2007? Unamfahamu Joseph Konyi wa Uganda? Angalia Goma pale Kongo. Hivi kweli wazuru wamechoka kuwaona wafrika wenzao! Sina uhakika Msumbiji hawapendi majirani kufika kwao. Dafful na Somalia hawapendi amani? Muamar Gaddafi alichokwa na wananchi wake mpaka kuamua kumuua kweli? Kiti cha Mugabe hakina mrithi? Hapa nasikia Nkurunzinza ni Raisi wa kuchaguliwa. Mseveni bado hajastaafu. Mwingine kaombwa kuwepo mpaka 2035!
Haya ndiyo maisha ya Afrika na mwafrika. Tunaishi kama mafahali ndani ya zizi moja. Hatufikirii mataifa yetu na bara letu. Bali fitina,chuki,hiuana na kila baya liende kwa ndugu zetu. Sikushanga kuona mhubiri anayejiita mtabiri Bushiri wa kusini mwa Afrika kutabiri magumu juu ya Nchi kama Tanzania. Ndiyo angefanya nini angali damu yake ni nyeusi kama ngozi yake? Mjasiri haachi asili. Je yeye kama mtu wa mungu anaihubiri afrika ama ana hubiri habari za mungu ili dunia iweze kupona?
Maendeleo,maarifa,vipaji na ubunifu vya waafrika vipo mirukoni mwa ubinafsi,chuki na wivu. Afrika inateketea kwa ubinafsi,chuki na wivu. Tunahitaji kupigana vita dhidi ya ubinafsi,chuki na wivu na tukiishinda vita hiyo ujinga,njaa na umasikini vitaogopa na kutukimbia kama yule Raisi wa moro alivyokimbia jeshi la Afrika.