TIMIZA NADHIRI ZAKO

Nadhiri ni ahadi anayoweka mtu, mbele za Mungu kwa maombi maalum kuwa atatimiza endapo Mungu atamfanyia jambo Fulani. Kuna mistari mingi katika Biblia inayozungumzia kuhusu nadhiri. Hebu tuchunguze kuhusu nadhiri na umuhimu wa kutimiza ahadi/nadiri. Timiza nadhiri zako kwa sababu zifuatazo:
NADHIRI NI AGANO/MAPATANO

Nadhiri huwekwa kwa Mwenye nguvu na mwaminifu wa kutimiza, Mungu wa Mbingu na nchi ndiye mtoshelevu wa kutimiza nadhiri.

Mfano: 1Samwel 1:11 Hana Mke wa Elkana aliweka nadhiri mbele za Mungu kwa kukosa mtoto;Akaweka nadhiri kuwa kama Mungu atampatia mtoto wa kiume ndipo naye atampatia mtoto hiyo Muda wote wa maisha yake. Baada ya Mungu kujibu maombi yake ndipo Hana akatimiza nadhiri yake. Kwa kumpeleka mtoto mbele ya Eli, kuhani huko Shilo. Hana alitimiza nadhiri yake Mimi na wewe tutimize nadhiri.

NADHIRI NI MAOMBI YENYE NGUVU 

Nadhiri huwekwa wakati wa sintoeleweka inapotokea kwa MTU, mfano vita, magonjwa, habari n.k Yakobo alimwekea MUNGU nadhiri wakati alipomkimbia Esau. Alimjengea Bwana madhabahu Mwanzo 28:20, mwanzo 35:7 Tunaona Yakobo akatimiza nadhiri wakati wake wa Kufanikiwa.

MUNGU HAWI RADHI NA WAPUMBAVU (Mhubiri 5:4)

Kwa vile nadhiri ni AGANO maalum kati ya Mungu na mtoto wake atamwadhibu yule asiye timiza. Mara NGAPI watu wsmeahidi kutekeleza mipango kwa kazi ya Mungu lakini baada ya MAFANIKIO wanajisahau? Timiza nadhiri zako.

Mpendwa msomaji wa makala hii wewe umeweka nadhiri Mara NGAPI ukashindwa kutimiza

Ubarikiwe mpendwa timiza nadhiri zako.