Ndoto ya kila mmoja ninayeongea naye ni kuwa tajiri na kumiliki mali nyingi. Na wengi huamua kujituma au kujiwekea malengo mbalimbali ya kuongeza kipato chao. Lakini pindi kipato kiongezekapo hujikuta na matumizi yakiongezeka mwisho wake kishindwa kufikia malengo yao ya kuwa matajiri au kujikusanyia mali. Mwisho wake huanza kukata tamaa na kuamini kuwa utajiri mgumu na wengine kuishia kujiingiza katika vitendo visivyo salama kwa lengo la kujipatia utajiri. Je, umewahi kujiuliza kwa nini hauwi tajiri ilihali unakipato kizuri? Ungana nami nikupeleke kwenye sheria za kukufikisha kwenye kuwa na mali nyingi na kuufikia utajiri ambao umekuwa unautamani kwa muda mrefu;-1:Tunza kipato chako;
Kama unalengo la kuwa tajiri ni lazima uweke ulichopata ndani jalafu utoke kutafuta kingine. Hicho utakachoweka hakikisha hakitoki kwa hali yeyote ile. Ndiyo kisitoke namaanisha bajeti zako zisihusike na sehemu hii ya ulichoweka. Na hicho unachoweka kisishuke kwenye moja ya kumi ya kipato chako. Kama kwenye nyumba za ibada unapeleka moja ya kumi na wewe jiwekee ndani moja ya kumi au zaidi halafu kiasi kinachobakia pangia matumizi yako mengine. Kwa mfano unakipato cha elfu thelathini kwa mwezi, hapo moja ya kumi itakuwa elfu tatu hii hakikisha umeiweka na usiitumie hii ndiyo sheria kuu katika kuelekea utajiri. Kwa nini ushindwe kuweka elfu tatu? Kama elfu ishirini na saba haijakutosha elfu tatu itatosha nini? Weka hiyo uone jinsi inavyoufikia utajiri. Nausisahau kurudi hapa kuwambia na wengine juu ya sheria hii.
2: Mali itafute mali nyingine;
Kwa nguvu zako huwezi kuwa na kasi ya kuzali mali kwa wingi kiasi cha kutumia muda mfupi kukusanya nyingi. Weka mali kama mbadala wako katika kufanya kazi zako. Kihalisia mali hufanyakazi kubwa kwa muda mfupi. Hivyo itakufanya kukamilisha mambo makubwa kwa muda mfupi na kuufikia utajiri. Mali pekee inauwezo wakuwaleta maadui pamoja. Hivyo mali inauwezo wa kukupa nguvu kazi kuliko nguvu zako. Iache mali ikutumikie, sio wewe uitumikie mali utaumia na makovu yake huwezi yaponya.
3:Kuwa na uwekezaji wenye macho;
Wengi wamefanikiwa kuufikia utajiri kutokana na hii sheria. Unapotaka kuwekeza hakikisha unawekeza sehemu sahihi zitakazo kutunzia na kukukuzia mali yako. Uwatafute wataaluma wa njia hiyo unayowekeza wakupe mawaidha ya uwekezaji wako na mbinu unazotakiwa kuzisimamia. Nakuhakikishia usisahau kuja hapa kuongea na wengine juu ya sheria hii.
4: Usifanye majaribio ya uwekezaji;
Unaanzaje kuweka mali kwenye jambo usilo na ufahamu nalo? Mbaya zaidi hujapata watu sahihi wa kukushauri juu ya jambo hilo. Hapa utakuwa unapoteza mali. Mali hukimbia mazimgira yasiyotumia jicho la ziada katika kuitunza na hasa kwa mtu anayetumia ulazima kutaka kuvuna hapo mali huwa haikai kabisa. Kuwekeza katika miradi usiyo na ufahamu na huna wenyeutaalamu na ujuzi wowote katika uwekezaji wako ujue mali haitakaa kwako. Wekeza sehemu unazoweza kuzifuatilia hapo utakuwa tajiri.
5:Usipokee ushauri huu;
Watu wengi wamekata tamaa ama kufa moyo wa kuufikia utajiri kwa sababu ya ushauri. Unafikiri unapata ushauri sahihi kwa ajiri ya kukuendeleza? Si kila mtu anao uwezo wa kutoa ushauri na si kila anyetoa ushauri basi ushauri huo huwa una kufaa katika maisha yako. Epuka kushauriwa na wapumbavu na wasio na uelewa juu ya jambo unalohitaji ushauriwe.
Kwa kuzingatia sheria hizo unaweza kuanza kuona ukipiga hatua za dhahabu sasa. Usisubiri ukwame ndipo uanze kukumbuka sheria hizo, japo siyo mbaya kukawia cha msingi ufike. Ila maisha yako yanakutaka uchukue hatua mara moja unapo ona njia sahihi.