UELEWA WAKO, NDIO UMASIKINI WAKO! par Mwl Philemon

Nafahamu dunia ya leo imekucha kila sehemu watu wanakazana kutafuta elimu. Katika kutafuta elimu huko umejitahidi umepata kacheti,stashahada au shahada. Sasa umerudi mtaani unakutana na watu wanaitwa maisha na Tajiri wakiwa wamekunja sura na hawaonyeshi dalili ya kutabasamu. Wewe na usomi wako unaendelea kuwatekenya na vyeti vyako bila mafanikio. Kila unapojaribu ndipo pagumu zaidi ya pale kwa jana. Pole ndugu yangu na shukuru kwa kukutana na mimi tabibu wa magunjwa yasiyo na tiba. Kwa kuwa na wewe unaugua magonjwa ya kukosa kazi, umasikini, utegemezi usiokuwa na kikomo, fikra zilizo na mipaka leo nataka upone. Kuna njia moja tu ya kupona na leo nitakueleza.

Ikane nafsi yako

Nafsi yako imekuwa ikikudanganya muda mrefu sana. Imekuaminisha mambo ambayo siyo kweli. Nafsi yako ina kuambia mambo kama;

Huwezi fanyakazi kama kuosha magari, kulima, kupiga rangi n.k eti kwakuwa wewe umesoma.

Nafsi inakwambia wewe ni mtu mkubwa huwezi kujidhariri hivyo.

Nafsi yako inakudanganya kuwa utapata kazi nzuri na itakupatia maisha mzuri.

Huo ni uongo mtupu amini usiamini hakuna kazi ndogo duniani. Kazi yeyote inayotoa thamani ya chochote sio kazi ndogo. Kila kazi inahitaji ubunifu ili kuongeza thamani yake. Unaanzaje kusema sio kazi ya hadhi yako angali unasubiri kazi za wenzio? Ina maana utumwa ni bora kuliko uhuru? Wenzio walibuni hizo kazi unazoona ni bora na wakazipa thamani ndio maana zimekuwa zilivyo sasa na umeanza kuzitamani.

(Kazi sio chanzo cha maisha mazuri ila kipato ndio hukuchagulia maisha)

Heshima kazi. Kama huna kazi na bado unaamini wewe ni mkubwa basi unajidanganya. Punda ni mdogo kwa umbo lakini anathamani kubwa mbele ya tembo kwa kuwa yuko meza kuu akila na kuishi karibu na binadamu. Na hakuna ajira imewekwa ili kukutajirisha. Kwa kuwa hakuna ajira isiyo na masharti. Na masharti hayo hayajari uwezo wako. Kujiajiri ndio ajira pekee unayoweza kutunga na kuvunja masharti utakavyo. Usikubari nafsi ikuendeshe,itakupeleka kwenye umasikini. Kumbuka hata ufanyekazi vipi huwezi pata maendeleo utumwani. Usichague kazi,chagua kipato unachohitaji ili ufanye kazi ya kukupatia kipato hicho. Hivyo kama utakuwa unauza pipi ya shilingi mia moja na unahitaji laki tisa itakubidi ukazane uuze pipi elfu moja. Kazi sio chanzo cha maisha bora ila kipato chako ndio hukuchagulia namna ya kuishi.