HITAJI LINAVYOTUMIKA KATIKA HATUA SITA(6) KUKUPA UTAJIRI. par Mwl Philemon.

Kabla hatujafikia kwenye utajiri kila mmoja huwa na njia zake za kupita kuelekea utajiri. Katika njia hizo unaweza kushindwa mara kadhaa. Usijari kuanguka huko, kumbuka kuanguka ni mwanzo wa kuafika uendako maana inakufanya kuijua njia vizuri na kuchukua tahadhari za kuepuka kudondoka kirahisi. Leo nakwenda kukupakulia hatua sita safi za kukufanya uwetajiri. Kwa nini ni hatua sita na kivipi utafikia utajiri kutokana na hatua hizi zilizoanza na hitaji lako la kutaka kuwa tajiri, ungana na mimi mwalimu wa maisha mazuri ninayekufundisha somo la mafanikio lisilopatikana kwenye mtaala wako wa elimu kuzichambua hatua hizo kama ifuatavyo;-

1:Tambua kiasi halisi cha fedha unayohitaji

Wengi tumeshindwa kufanikiwa sio kwa kuwa hatuwezi kufanikiwa au kwa kukosa bahati ya mafanikio hapana. Ila wengi tumeshindwa kufanikiwa kwa kuwa hatujui tunachotaka. Tatizo hili limekuwa kubwa na tiba yake ipo kwa watu wachache na moja ya watu hao wachache ni hapa mwenyenyumba kukaa hapa unapata tiba unayoihitaji kwa ufasaha zaidi. Pamoja na kutafuta kote unako hangaika ili uweze kufanikiwa hitaji lako liweze timia nilazima ubainishe unahitaji kuwa na kiasi gani cha mali au fedha. Kitendo cha kubaini kiasi unachohitaji ni hatua ya kwanza ya kutambua mafanikio unayoyahitaji. Usipotambua kiasi cha fedha au mali unachohitaji kuwa nacho ni sawa na kwenda safari usiyoijua. Ni vyema ukaanza kutambua safari yako itaishia wapi ama inaelekea wapi ndipo uanzekuisafiri sasa maana itakusaidia kutambua kasi ipi itafaa na baada ya muda gani utaumaliza umbali huo. Kwa kubaini kiasi cha fedha unacho hitaji itakusaidia katika hatua ya pili ambayo ni;-

2:Amua njia ya kukupatia unayoihitaji

Huwezi kufika unakotaka kama hujajua njia ipi utapitia. Kwa kuwa umeshaamua kupata fedha kiasi fulani basi ni vyema ukaamua ni kitu gani utafanya kuipata pesa hiyo unayoihitaji. Kwa kutambua kitu kitakacho kupatia fedha hiyo itakupawepesi kuelekea katika kutimiza hitaji lako la kuwa tajiri. Ni sawa na kutambua usafiri utakao tumia katika safari yako ambayo tayari uliiainisha katika hatua ya kwanza kwamba unaenda wapi. Hivyo itasaidia kutambua kasi ya usafiri wako ambao utakusaidia kuamua hatua ya tatu ambayo ni;-

3:Teua muda utakaotumia kupata fedha hiyo

Kwa kuwa umeshabaini kiasi cha fedha unachohitaji na ukawianisha na kitu cha kukupatia fedha hiyo, amua ni baada ya muda gani utakuwa tayari unafedha hiyo unayoihitaji. Hii itakufanya kuwekeza muda na juhudi zako katika kukamilisha hitaji hilo lililo mbele yako kwa kuwa mipango yako ndio itakuongoza katika kuendea hitaji lako. Baada ya kutenga muda wa kupata fedha ambayo ni hatua ya tatu utafuatia hatua ya nne ambayo ni;-

4:Weka mpango na uutekeleze mara moja

Baada ya kuwa umebaini kiasi cha pesa unachohitaji, ni kitu gani kitakupatia fedha hiyo na lini utakuwa umepata sasa pangilia namna ya kutekeleza mambo hayo kwa wakati sahihi na baada ya kupangilia usisubiri, anza mara moja kuufanyia kazi mpango huo kuelekea katika utajiri.

5:Andika mtiririko huo wa maelekezo kutokea hatua ya kwanza hadi ya nne

Andika katika kitabu cha kumbukumbu mambo uliyouaamua katika hatua zote nne za mwanzo. Hii itakusaidia kuwa na taarifa isiyofutika hivyo kufanya malengo yasipotee kirahisi hivyo kuweza kutumika kwa muda mrefu bila kupoteza dira yake. Baada ya kuyaandika ni vyema ukaifuata hatua ya sita ambayo ni;-

6:Isome taarifa hiyo mara mbili kwa siku, mara moja asubuhi na nyingine usiku

Kwa kuisoma taarifa yako kwa vipindi hivyo itakuwa inakaa kichwani na itakuwa kumbukumbu nzuri ya nini unahitaji katika maisha yako kwa wakati huo unaohusika kulingana na mipango uliyojiwekea. Asubuhi itakukumbusha yapi unapaswa kwenda kutenda kwa siku hiyo na kusoma usiku kutakupa nafasi ya kuitafakari kwa mapana mipango yako kwa siku iliyopita na siku inayofuata.

Kumbuka kuanguka ni mwanzo wa kufanikiwa.