Yohana 15:7-10
“Ninyi mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lolote mtakalo nanyi mtatendewa” Soma vizuri katika tafsiri nzuri ya Amplifier Bible, inasema “mkiishi ndani yangu… na maneno yangu yakidumu ndani yenu na kuendelea kuishi ndani ya mioyo yenu…)
Ukiona mtu anatangatanga, ukiona mtu anazini na nabii au mtume, ukiona mtu anazurura kutafuta muujiza au uponyaji, ukiona mtu amefungasha maji, chumvi, vitambaa, mafuta, ndala, mchanga, na takataka za kila aina kama aliyetoka kwa mganga wa kienyeji, ujue shida ipo hapo! “KUISHI NDANI YA MUNGU NA MANENO YAKE KUISHI NDANI…” Haiwezekani uishi ndani ya Mungu na bado unatapeliwa kwa jina la huyo Mungu!, Jiulize, hivi akili zako ziko sawa? Yaani wewe unaishi ikulu ya nchi alafu unababaishwa au unamtetemekea mwenyekiti wa serekali za mtaa? Hivi unajua wewe ni Mungu, wewe ni mtoto wa Mfalme, wewe mwenyewe ni nabii wa maisha yako!
Lakini pia lazima uelewe, unaomba au kutafuta lolote lipi? Maana usiwe unalazimisha kumpata Sauli badala ya Daudi, mwanafunzi wa darasa la saba unalazimisha Mungu akupe mume, unafunga na kuomba kijijini kweni ufanyike muujiza wa kutua ndege wakati hata uwanja wa ndege hakuna…
Nikiwa kama msomi wa Biblia naelewa sana kuhusu matumizi ya baadhi ya vitu kama mafuta, lakini pia naelewa kabisa kwamba Roho wa Mungu anaweza akaleta ufunuo fulani kwasababu maalum. Shida ni kwamba, watu wamepindua maandiko, nyuma ya pazia ya matumizi ya baadhi ya vitu si ya ki-Mungu. Nataka uelewe kwamba “PERSONAL REVELATION IS NOT A DOCTRINE”
TUPO KWENYE KIPINDI KIBAYA SANA. Watu wanapewa kila takataka hadi sumu kwa jina la muujiza. Watu wamelishwa majani, nyoka, kuvalishwa ndala, kuvuliwa singlendi na soksi za muhubiri, kupuliziwa dawa ya mbu na mende…
Sikiliza; UNABII WOWOTE AMBAO UPO KINYUME NA MAANDIKO HAUFAI, NI UGANGA, NI UCHAWI TENA NI USHETANI KABISA.