
Hatukuumbwa na ukamilifu wa vyote. Si kimwili,kihali wala kimali. Hivyo tumekuwepo kwa ajiri ya kujisaidia na kusaidia wengine katika nyanja mbalimbali za kimaisha. Kulingana na hilo unapaswa kuchagua aina ya watu wanaokamilisha mzunguko wa kusaidia na kusaidiwa. Ukipata hao wang’anganie wasiondoke kwako.
Nipo hapa kukuonyesha aina marafiki na ndugu wasiokufaa kuendesha nao maisha na kujenga mahusiano nao;-
1:Wanaopenda kutendewa tu
Kuna watu wao toka waumbwe hawajawahi kutoa kwa kumpatia mwingine, hupenda kiingie kwao tu. Si wawazo,mbinu wala mchango. Wapo na wewe kwa lengo moja la kuvuna kutoka kwako. Huwezi kuweka kitu wakaona na wasikupe shida zao na wewe unapokuwa na shida wao hukaa mbali. Hawa ni watu wa kuwaepuka sana katika maisha yako.
2:Wapenda starehe kuliko kazi
Starehe ziliwekwa kwa lengo la kumpumzisha na kumrejeshea uwezo wa kutenda tena,mtu aliyechoka. Sasa inakuwaje uitangulize kabla hujachoka? Unapokuwa na watu wanao tanguliza starehe kabla hawajachoka jua mnajiandalia umasikini wa kudumu. Hivyo usiwakaribishe jirani na wewe watu wa aina hii. Hawakufai hata kidogo. Ni kheri kufuga mbwa asiyewinda anaweza kubwekea wezi lakini siyo mtu anayekupa mbinu za kutumia tu kila kunapokucha hujiulizi yeye anatafuta muda gani mpaka kaw na zakutumia? Anakujengea matatizo ambayo hutaweza kuyatatua kamwe. Mtu wa mtindo huu ni wakuepukwa sana unapotaka kuimarisha uchumi wako.
3:Wanafiki na wambea(Wapelelezi)
Usiombe hata kuwafahamu watu hawa. Huwezi kuweka mpango au wazo na wao lisiwekwe wazi. Ukipanga nao hapa wakigeuka mgongo wanapanga na wengine namna ya kuzuia mpango huo usifanikiwe kama hawa kupanga hivyo basi wataufikisha kwa maadui zako hivyo kuandaliwa bomu la kuilipua pindi utakapoanza kutekeleza mipango hiyo. Kwa nini uwenao sasa watu kama hawa? Waepuke tafadhali kutokufanya hivyo ni kujichimbia kaburi lako ambalo hutazikwa na sanda, kwa maana ukapuku hautacheza mbali na wewe.
4:Wavivu na wakatishaji wa tamaa
Hawa ni marafiki wasio na mbele wala nyuma. Wamejaa maneno ya fungu la kukosa kuliko mawazo ya kufanikiwa. Hushinda wakiwaza na kujadili mafanikio ya wengine. Unapokuwa na wazo lako la kushauriwa wao huonyesha upande wa kushindwa zaidi na huwa na mifano mingi ya kushindwa kuliko namna ya kufanikiwa. Huhitaji kabisa watu wa aina hii kuwa karibu yako unapotaka kujijenga kwani hutaweza.
5:Wapinzani wasio na mafanikio
Unahitaji mpinzani mzuri ili uweze kujiimarisha vizuri ukimpata jenga ukaribu naye ili upate mbinu zaidi na zaidi. Mpinzani asiyependa maendeleo na asiyeendelea hakufai kabisa katika kijijenga kwako. Maana itakuwa sawa na kupambana na ukuta ambao huwa hausogei na huwezi kuusogeza pia hivyo aidha ubaki hapohapo au uuvunje upite na kusogea mbele. Mimi na chagua kwa niaba yako pia uvunje uhusiano(ukuta) na mtu asiyeendelea na anazuia kufanikiwa kwako hana madhara huyo. Wanini unamkaribisha mpinzani wa namna hiyo katika maisha yako sasa?
6:Anayejua kila kitu(asiyependa kujifunza)
Elimu tuliwekewa kwa lengo la kuongeza au kubadili mitazamo yetu ili tuweze kuwa na mipangilio isiyokuwa na mawimbiwimbi sana. Sasa unapokuwa na rafiki mjuaji atakupeleka pabaya maana hata kama hana uhakika na analolitenda bado huwa king’ang’anizi wakutaka muendelee bila kujali hasara ya mali na muda mnayoweza kuipata mbeleni. Hapendi kuongeza maarifa mapya na hana maarifa ya kutosha. Si rafiki mzuri maana hatakuwa na tabia ya kufikiri,kusikiliza na hukurupuka katika maamuzi. Usimpe nafasi katika maisha yako mtu wa mtindo huo nakwambia. Atakuzamisha na unaweza kujikuta unatengwa na watu walio sahihi na wenye mitazamo makini.
Nakukumbusha aina hizo sita za ndugu na marafiki waepuke. Hutaweza kijijengea maisha yako mbele yao na ukafika utakako.
Ni lugha ipi ambayo wewe unatumia zaidi?
J’aimeJ’aime
Kirundi na kifaransa ila ukitaka kuwasiliana unaweza ukatumia kingereza
J’aimeJ’aime