Shalom Shalom!Ni siku nyingine njema Bwana ameweka kwa ajili yetu msomaji ,kabla ya yote tumushukuru Mungu;
Baba yetu uliye mbinguni juu twalitukuza jina lako ,twalisifu maana umeinuliwa juu sana na wewe niwa ajabu. Asante kutulinda na kutubariki na neno lako .Tutembelee siku ya leo tukuone tena katika jina la Yesu Kristo,Amina!
Ndugu dada ambaye unasoma tunakusalimia katika jina la Yesu Kristo!
Leo tunazungumzia neno : USIOGOPE.
Tusome kitabu cha Nabii lsaya 44:2
» Mimi Mwenyezi Mungu Muumba wako niliye kufanya tangu tumboni mwa mama yako nimekuja kukusaidia wewe. Mimi Mwenyezi Mungu nasema Usiogope ewe taifa la Yakobo ,mtumishi wangu,naam Usiogope Yeshuruni mteule wangu.
Twendanishe na lsaya 43:2
« Mkipita katika mafuriko ,mimi nitakuwa pamoja nanyi ; mkipita katika mito haitawashinda nguvu. Mkitembea katika moto hamtaunguzwa:Mwali wa moto hautawaunguza. »,Halleluya!
Lengo la leo ni kukutia moyo na nguvu wewe msomaji wetu ikiwa we ni mwanaburundi au yeyote yule anaelewa lugha ya kiswahili; wewe uko jela nchini Burundi ninawajua wengi wako huko,wewe labda ni mkimbizi yatima au mjane na uko huko Nyarugusu,Mtenderi Tanzania,labda uko Mahama Rwanda,Nakivale ,Chaka huko Uganda au Kakuma huko Kenya,Nampula Mozambique na kokote uliko kwa shida Mungu amesha sema Usiogope.
Ulifanikiwa kufika huko kumbuka kuna wengine hawakuweza. Nataka nikutie moyo ya kwamba Mungu hakukusahau hata kidogo yeye kasema anakuja kukusaidia maana alikuumba ,anakujua uko katika hizo shida,amini neno lake utaona mabadiliko.
Upitapo katika mafuriko,mito na moto haya hayatakupeleka. Fikiria vizuri; je wewe kufika hapo ni nguvu yako? Hapana Mungu bado anakupenda ni Baba yako. Wengine walikufa hata kama uko hapo shukuru Mungu kwanza. Ahadi yake haiozi na ni Ukweli ,ni amina !Kesho utasema ameni kubwa ukirejeshwa katika nchi yako,katika hali yako.
Nikiwa kijana shalobaro sekondari nimewahi pigwa lisasi na wanajeshi enzi hizo mwaka 2005 nikienda shuleni na hakuna hata moja ilinigusa. Lakini nikamnung’unikia Mungu. Je kwanini Ee Mungu hukunipeleka Marekani au Ulaya katika nchi zimeendelea bali ukaniweka Afrika hasa Burundi mahali pa vita hivi?
Mungu hakusita kunijibu akaniambia : Nitakulinda ,nimekuweka ili uwe ambasada wangu yaani Mbalozi wangu .Dah! Sikuelewa ni nini Mungu anazungumzia lakini niliposoma neno la Bwana katika kitabu cha Yeremiya 1:5 nikaelewa.
« Kabla kujachukuliwa mimba ,mimi nilikujua ,Kabla hujazaliwa ,mimi nilikuweka wakfu ,nilikuteua uwe Nabii kwa mataifa . » Halleluya!
Mungu amekuteua amekuweka ili uwe nabii kwa mataifa ndiyo maana wengine walikufa wewe bado upo.
Kuna aina ya watoto wameniambia kwamba kuzaliwa kwao kumekuwa ajali au makosa. Mama alibakwa labda, au hakutaka kuzaa lakini shida ikatokea akazalishwa na mpenzi wake ,boss wake akatupwa au akanyanyaswa hivi na vile unajua shida ni nyingi hapa duniani. Sasa matokeo ni wewe unasikia haupendwi,uko barabarani hakuna wakukujali,mama hayuko,baba hujawahi mwona yaani maisha ni taabu tu unalala chini ya daraja.
=> Sikiliza kwa makini Mungu amesema kabla hujachukuliwa mimba alikujua,kabla kujazaliwa alikujua,anakuja kukusaidia . Kuzaliwa kwako si makosa au ajali bali mpango wake.Mungu haumbi kimakosa!
Jambo tu anataka kwako ,ni wewe uelewe Mungu ,umjue ujue kwamba ni Mkuu anaweza. Usiogope sasa inuka ; Kitu nakuomba tu tembea na yeye,tubu dhambi zako wewe ni Nabii kwa mataifa. Kesho tutaendelea na mada hiyi usikate tamaa Mungu anakupenda sana. Mungu akuonekaniye kwa njia ya ajabu leo katika jina la Yesu Kristo! Amina.