Bwana Yesu asifiwe sana! Nawasalimu katika jina la Yesu Kristo aliye mfalme na mwokozi wetu!Tuombe: Baba uliyetukuka katika jina la Yesu Kristo twalisifu na kulitukuza jina lako takatifu siku ya leo. Ni asante kutuumba na mipango yako miema iti tutende mapenzi yako. Twakuhitaji Ee Bwana usiku na mchana uwe nasi hadi milele katika jina la Yesu tumeomba na kuamini,amina!
Jina langu ni Mchungaji Uwisezerano Libéré!
Leo tunaendelea na ujumbe wa jana : USIOGOPE.
Tusome waefeso 2:10 na 1:4
« Maana tu kazi yake ,tuliumbwa katika Kristo Yesu tutende matendo mema ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo. »
1:4″ Kama vile alivyotuchagua katika Yeye kabla kuwekwa misingi ya ulimwengu ili tuwe watakatifu watu wasio na hatia mbele zake katika Pendo. »Halleluya!
Bwana apewe sifa!
Maana yake usiogope ni uwe mjasiri,usonge mbele na usirudi nyuma.
Neno katika kitabu cha waefeso limetwambia kwamba kabla ya misingi ya dunia kuwekwa Mungu alituchagua,alituteua wewe na mimi ili tuwe watakatifu wake bila hatia yoyote.
Kilichotufanya kutotembea katika njia iliyohaki ni shetani.ibilisi anajua ni nini ufalme wa Mungu kwani alikuwa mbinguni; usijifanye ibilisi anajua yale matendo mema tuliumbiwa. Kwa kuwa yeye na mamalaika wake (ndiyo mapepo leo) walishahukumiwa wanataka tuchangie moto wa milele huko ziwani la moto. Soma Ufunuo 20:10.
Kabla Burundi kupata uhuru shetani alituchezea sana ,nasi tukasahau yakwamba matendo alituumbia Mungu si chuki ya kikabila hadi kuuwana na kuteketezana. Wewe labda ni muhutu,mtutsi au mutwa,kwa nini umuchukie mwenzio? Aliyekuumba wewe ndiye aliumba huyo rafiki yako. Je kuna sababu yote ya kumuua?
Harafu tukimaliza tunaingia makanisani na misikitini tunadai tunamuabudu Mungu,wa wapi? Acha unafiki ndugu yangu,hauendi mahali popote.
Vyama vya siasa vimekuja kukwambia yule si wa chama chetu ni adui,gonga na utoe uhai kabisa. Sijui mwingine ati yule si mwanamkoa wetu kwa hiyo hastahili kukalia kiti hiki tutafute wa kwetu,nani kasema?
Wengine ati huyu si wakabila yetu fukuza kwa shamba lake tulichukuwe,nakwambia we ni mwizi.
Katika makanisa na misikiti vyama vikaingia ati huyu kiongozi si wa chama tawala sasa tufanye njama atoke,mgawanyiko na mapigano ndivyo hivyo ,jamani.
Yule mwingine tumnyime haki,kazi hapati si kabila yetu,si mwanachama,si mwanamkoa …Huyu asipokubali kulala na mimi kazi simpi. Haya yooote ni mambo tumekuwa tunatenda ya kishetani hayampendezi Mungu,hatukuumbiwa hivi!
Mwanaburundi au yeyote unaposoma popote ulipo mtu wa moyo huyu,mtu wa mwenendo huyu hataingia Burundi mpya maana bibliya inatwambia ya kwamba Mungu alituumbia matendo mema kabla ya dunia kuwekwa ili tuenende nayo.
Je katika hizi chuki za ukabila ,vyama ,ubaguzi wa mikoa ,kunyanyasana na kuuwana hovyo ni kusudi lake Mungu au ni matendo yake machafu ibilisi?Acha maovu,tenda mema,badilika .
Tusome 1Wafalme 18:21 na 38.
» Naye Eliya akawakaribia watu wote akanena ,Mtasita-sita katikati ya mawazo mawili hadi lini?
Bwana ikiwa ndiye Mungu mfuateni: Bali ikiwa baali ndiye Mungu haya mfuateni yeye.wale watu hawakumjibu. »
38. »Ndipo moto wa Bwana ukashuka ukaiteketeza sada yake ya kuteketezwa na kuni na mawe na mavumbi yote ukayaramba yale maji yalikuwamo mfereji.
Ndugu dada ikiwa umenifuata kwa makini ,Mungu niwa ajabu hatuna cha kumlinganisha.
Mukuje tumfuate yeye tufanye mapenzi yake kama vile nabii Eliya alisema akiambia Ahabu na watu wake.
Lakini yule yeyote sijali kabila au chama ,ikiwa bado ana chuki ndani yake kumhusu ndugu ye,asipotubu kuna moto hivi punde unakuja utamlamba. Chama ulikifanya kuwa mungu wako,kuna moto. Bibliya inatwambia kwamba amchukiae ndugu ye ni muuaji,ikaongezea kwamba mshahara wa dhambi ni mauti.Acha chuki tenda mema ,tubu,omba Mungu atakusamehe,atakusaidi ndiyo uingie Burundi mpya.
Yesu kasema « mpende Mungu wako na akili yako yote na maisha yako yote. Na umpende jirani yako kama unavyo jipenda mwenyewe. »
Umpendao hautamuua ,hautambaka,hautamnyima haki ,hautamfanyia njama ,hautamzini ,hautamnyanyasa ,nkt! Epuka matendo hayo tutende mapenzi yake Mungu aliyetuumba na upendo katika Kristo.
Ikiwa hauna lawama mbele zake Mungu usiogope muda ujao atakupigania.
Ubarikiwe sana unapotii neno hili,Mungu asifiwe.Amina!