Bwana Yesu mwokozi wetu asifiwe sana!Ni siku nyingine tena twamshukuru Mungu kutujalia.
Tuombe: Baba uliye mbinguni usifiwe na upewe abudu zote takatifu maana hakuna muweza kama wewe Jehova. Ni asante kutupatia uhai nawe ututumie vile upendavyo katika jina la Yesu Kristo tumeomba na kuamini,amina.
Mchungaji Uwisezerano Libéré ndiye mtumishi.
Leo ningependa tukumbushane yale Mungu amekuwa anazungumzia wanamaombi mbali mbali. Mada ya leo tunaweza yiita :UKUMBUSHO l.
Tusome Yeremia 33:3
« Niite nami nitakujibu na kukwambia mambo makubwa yaliofichika ambayo hujapata kuyajua . » Halleluya!
Bwana asifiwe sana! Neno hili Mungu alimjibu Nabii Yeremia kutokana na na wakati mugumu alikuwa nao mara kuteswa mara kuzuiliwa magerezani.
Nasi tumekuwa na nyakati ngumu sana myaka si kidogo,ndio Mungu akazungumzia watu kadhaa toka sehemu mbali mbali za dunia. Kuna yale tumeshashuhudia na mengine bado tunaomba atimizwe.
Ni vizuri kukumbushana hapo ndipo hata wale ambao hawajajua wanaweza jua yale Mungu alizungumza.lkiwa wewe una shaka na yale tunakutangazia leo,chukuwa nafasi umwombe Mungu atakufunulia yaliofichwa.
-Mungu alizungumza kwamba mataifa ataketi na kujadiliana kuhusu mgogoro wa Burundi katika mambo ya kisiasa na jeshi lakini watashindwa.
-Mungu alisema,ataiibuwa chemchemi ya uvuvio nchini Burundi miujiza na maajabu vitatendeka ,mataifa mengine takuja kuchota kwenye uvuvio huo na wateule wake Mungu wataipeleka injili nje wakihubiria watu kumurudia Mungu.
-Nyakati hizo ,wanaburundi wote,ngeli zote,makabila yote ,dini zote,sehemu zote za nchi watamuabudu Mungu katika ukweli na Roho,bila kujali utofauti wao kwa sababu watakuwa wamekwishajionea miujiza atakayo kuwa anatenda.
-Mwaka 1971 Mungu alizungumzia kuwa nchi ilikuwa inaelekea kupata taabu ,watu waliuana damu ikamwagwa wengine wakakimbia nje. Imekuwa hivo mwaka ulifuata 1972 watu zaidi ya laki tatu wakapoteza maisha na wengine wapatao mlioni moja wakakimbilia Tanzania,Rwand,Zaire(Congo ) na pengine mbali.
-Mwaka 1973 Mungu alianza kuzungumzia ahadi halisi na ukombozi wa nchi akifunulia wanamaombi wakimbizi nje na wakimbizi walikuwa kwenye misitu mbali mbali kipindi hicho.
-Mwaka 1979 kulikuwa mama raia wa ubeljiji Mungu alituma kutafuta wateule wake na akasema vile Mungu alisema. Alizungumzia uchaguzi na vita vitakavyo ibuka kufuatia mauaji ya maraïs wawili watakao uawa. Kama mnakumbuka (Raïs Ndandaye Melchior 1993 na Cyprien Ntaryamira 1994)
Mwaka 1984 sehemu za Nyakabondo kijijini Rubirizi tarafani Mutimbuzi Mkoani Bujumbura,wanamaombi Mungu aliwambia kwamba kutakuwa maraïs watano(5) wakihutu nchini Burundi. Na huyu wa mwisho atajiongeza muhura. Mgogoro utaanzia hapo ,maandamano na shamburizi vitanza mjini Bujumbura na kidogo vitashika nchini kote hadi Mungu atakapo jitukuza na kutimiza ahadi yake,ataleta amani tele mwenyewe.
Mungu niwa ajabu ndugu yangu,tumusifu na kumuamini ,ni Muweza yote.
Kutabu cha Nabii Amos 3:7
» Hakika Bwana Mwenyezi Mungu hafanyi kitu bila kuwafunulia watumishi wake manabii nia yake.
Tutaendelea kesho ,amani iwe juu yenu muendelee kumwomba Mungu ni mwanimifu sana. Mbarikiwe sana!