Mungu mwenye enzi zote ashukuriwe kutufikisha siku ya leo tarehe mosi mwezi Agosti tayari tumeingia kwa neema yake tu. Baba tunalisifu na kulitukuza jina lako Eee mwenye enzi . Kando yako hakuna Mungu mwingine ,uwe pamoja nasi mwezi huyu utushindie ,yale ulioandaa kwa ajili yetu atendeke na yale shetani aliotupangia nayavunja nayaharibu ni katika jina la Yesu tumeomba na kuamini,amina!
Lengo letu la mwezi huyu ni IMANI.
Mada yetu leo ni lmani l.
Tusome Waebrania 11:1
« Kuwa na lmana ni kuwa na hakika ya mambo tunayotumainia; kusadiki kabisa mambo tusioyaona . » Halleluya!
Imani ni kitu muhimu. Haionekani si kitu unawezagusa ila lmana yako inaonekana kwa matendo yako. Ikiwa unaamini Mungu una uhakika ya kwamba alichokisema ,alichoahidi atatenda.
Kuna maneno mawili ya kushika katika somo hili:
1) Kuwa na hakika ; ( kwa lugha ya kimombo:Having assurance).
2) Kusadiki: Kuwa unayaona mambo hayo kama picha katika roho.
Mfano: Kuna wimbo tulitengeneza na rafiki yangu tangu 2014 usemao « Unapendeza ». Tukasema Umependeza taifa letu hatukuimba vile tunaona sasa.Hapana! Tumeimba ,tukachukuwa picha kwa lmani ya mambo tunayoyatarajia ,tunayoyatumainia nchini mwetu,Halleluya!
Tayari bibliya lmesema kusadiki mambo tusiyoyaona ,kuyachukuwa kama ukweli na kunza kutembea kama uko ndani yake.
Natak leo usitize kulia ,kunung’unika ,komesha roho zinazokwambia hautaweza . sema mimi ni mshindi ,nitaishi kwa lmani.
Waebrania 11:6
« Basi pasipo lmani haiwezekani kumpendeza Mungu. Kwa maana kila mtu anaye mwendea Mungu ni lazima aamini kwamba Mungu yuko ,na kwamba huwatuza wale wanaomtafuta.. » Halleluya!
Mtu yule ambaye hana lmani hampendezi Mungu ,Mungu hawezi mtambua . Ni lazima uamini kwamba:(1) Mungu yupo,(2) unapo muamini atakutuza katika ahadi yake.
Atakutendea mema,atakubariki ,atakutimizia ahadi,atakulinda ,atakujali hata ukifa bila kuiona ahadi atawapatia watoto wako na wajukuu.
Kuna manufaa ya kuwa na lmani:
1)Ukiwa na lmani unakubariki . Webrania 11:4.
2) Ukifa ukiwa na lmani bado inanena ,itafanya kazi. Waebr 11:4
3) Ukiwa na lmani unampendeza Mungu. Waebr 11:5
4) Ukiwa na lmani unatii Mungu. Waebr 11:7-8.
5) Ukiwa na lmani huwezi kufa hovyo. Waebr 11:7
6) Ukiwa na lmani unakuwa muadilifu. Waebr 11:7
7) Ukiwa na lmani unatimiziwa ahadi. Waebr 11: 11.
8) Ukiwa na lmani unajaliwa neema. Waebr 11:11
Imani ndiyo ilisababisha Yoshua kunena kwamba maadui zao watawakula kama mkate,kama chakula ingawa rafiki zake wapelelezi waliambia wanalsraeli yakwamba hawawezi ingia katika ile nchi,wao ni kama sisimizi mbele zao. Lakini mwenye lmani Yoshua aliingia nakupigana vita kwa lmani akawashinda mpaka akasimamisha jua.
Soma Hesabu 14:9
» Lakini msimwasi Mungu Bwana wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi ,maana wao nikama chakula kwetu,uvuli uliokuwa juu yao umeondolewa,naye Bwana Yu pamoja nasi; msiwaogope!
Nakwambia leo huisha lmani yako usiwogope wale waliogeuza nchi yetu kuwa shamba lao maana Mungu Yu pamoja nasi. Uvuli ulikuwa juu yao ulishaondolewa,shetani alidanganya watu ati hawawezi ingia kumbe nguvu yetu siya kimwili bali nguvu Yetu ni Mungu.
Tafakari hayo siku ya leo ,uanze kumuamini Mungu. Tukutane kesho tena kwa majaliwa ya Mungu tuendeleze mada hiyi ,ubarikiwe unapoanza kuiona nchi mpya,Burundi mya kabla tuende mbinguni. Amina!