Ukumbusho kwa yale Mungi amezungumuziya tayifa la Burundi

Tunamsifu Mungu Bwana wa majeshi kutuzawadia siku hii tena ili mapenzi yake afanyike.
Tuombe: Baba uhimidiwe na uabudiwe maana kando yako hakuna Mungu mwingine. Tunaomba uwepo wako uwe nasi kwa siku ya leo na utubariki katika jina la Yesu Kristo. Amina!

Bwana asifiwe sana! Leo tunaendelea na mada yetu ya Ukumbusho kuhusu mambo Mungu alizungumuzia watu kadhaa wanamaombi kuhusu ahadi yake .

Tusome Yeremia 29:11-12.

« Maana mimi Mwenyezi Mungu ninajua mawazo ninayo wawazia ninyi,asema Bwana,ni mawazo ya amani wala si ya mabaya kuwapa ninyi tumaini siku za mwisho.

12.Nanyi mtaniita ,mtakwenda na kuniomba nami nitawasikiliza . » Halleluya!

Ndugu dada unayesoma nakala hiyi ningependa uelewe ya kwamaba Mungu ni amani ,Mungu ni upendo mipango yake kwetu ni mizuri ila shetani alikuja na kuharibu kazi zake Mungu. Mungu hakukusudia nchi yetu iwe hivi ilivyo sasa,Hapana! Maana anajua mawazo anayotuwazia ; ni mema si mabaya ,aliyeleta ubaya ni yule mwovu. Ndiyo maana Mungu katoa ahadi kasema nitawakomboa.

Huyu mstari wa 11 mwisho wake unaona ; akisha tupatia amani ,tuwe na matumaini ya siku za mwisho tutamuita ,tutamuabudu naye ataitika,atasikiliza sifa na abudu vyetu. Halleluya!Haya mambo bado hayajafanyika nchini mwetu ndiyo maana Mungu yaja haraka kutusaidia wateule wake .

Tuendelee na Ukumbusho wetu :

-Mwaka 1992 ,kuna kikundi cha wanamaombi Mungu alifunulia hivi:

1) Uchaguzi utafanyika mshindi atakuwa raïs ataongoza muda mufupi ,atakuja kuawa na wanaomlinda. ( haya tumeshuhudia mwaka 1993).

2)Atakayemrithi atakufia nchini jirani. ( Tumeshuhudia haya mwaka 1994 nchini Rwanda raïs Ntaryamira akifariki katika ndege moja na raïs wa zamani Habyalimana wakitoka jiji Arusha Tz).

3) Akikuja raïs mwingine atafukuzwa madarakani na aliyekuwa anaongoza nchi kabla ya hawa watatu kupata madaraka.(Haya tumeshuhudia mwaka 1996). 

4) Baadaye kutakuwa mazungumzo ya amani ,watachangia madraka lakini uongo na kupuuziana ndivyo vitatawala yale makubaliano yao,hayatadumu.

5) Kutakuwa uchaguzi atayeushinda ni raïs mwenye kujifanya sana yeye ni mcha Mungu lakini kutazuka machafuko ya ajabu.(Tumeshuhudia huyu tangu mwaka 2005 hadi sasa).

6) Mungu alisema ,kwa wakati msiojua ,baada ya watu kupoteza tumaini ,nitasimamisha jogoo wawili .Watapigana na ndimi za moto zitaonekana hewani nami nitanyamanza kwa sababu hawa wote wawili ni waovu.

7) Yule kiongozi wakale ,aliyejipatia madaraka kwa kufukuza yule raïs wa tatu,atadhaminia kurudi madarakani kwa kutumia kifua(nguvu) lakini atashindwa. Kuna watu watakuja kumsaidia na kujaribu kumlinda lakini atakufa.

8) Akasema waambieni kwamba huyu mgogoro wa Burundi hautadumu kwa muda mrefu kipindi hicho,ndipo nitasimamisha niliyempaka mafuta ufichoni kama Dawidi. Huyu ataongoza ,nami nitaamsha uvuvio. Mataifa mengine atashangaa kuhusu ushindi nitapatia wateule wangu.

Isaya 60:21-22.

9) Na mataifa atakuja kuchota baraka nchini humo na wateule wangu watajaa mataifa mengine wakihubiri injili njema. Utajiri ,amani na maendeleo ya ajabu yatashuhudiwa nchini Burundi kipindi hicho.

10) Katika huyu Uvuvio watu watajitolea sana na kufanya bidii kuhubiri injili.Kuna wale watakufia nchini lndia na nchi mbali mbali Asia,watachinjwa na shingo zao zitatolewa kwa sababu watakuwa wanahubi injili ya Yesu Kristo!

Mwisho!

__________℅_______

Ndugu ,dada unayesoma ujumbe huyu ,nakutangazia leo kama ulikuwa hujaamini ahadi yake Mungu ubadilishe msimamo wako. Leo ningependa nitie moyo wanaoshikwa na kupelekwa magerezani,mtatoka.wale wanaolilia familia zao nchini mtafutwa machozi hivi karibuni,Wale muna huzuni imeinamisha myoyo yenu chini ,Mungu anawawazia mema.lnuka amini Mungu nimwaminifu sana kwa kila jambo hautakufa bali utaishi uyatangazie mataifa injili njema ya Bwana ,Halleluya!

Soma zaburi 118:17.

Mungu awalinde ,awatendee mema na awakumbuke katika jina la Yesu Kristo,Amina!