Bwana Mungu asifiwe sana!Ashukuriwe Mungu wa majeshi kutupatia neema ya kuamka tena.
Baba jina lako likuzwe ,mapenzi yako afanyike leo ndiyo tutembee katika ukweli wako .Waponye wale wanaokuhitaji na ujidhihirishe kwa wale wenye imani haba katika jina la Yesu Kristo! Amina
Jina langu Mchungaji Uwisezerano Libéré!
Tuendelee na mada yetu ya lMANI II.
Leo ningependa tujifunze kuhusu lmani tukitumia mifano 3 Yesu alitumia kuonyesha mitume ya kwamba lmani nikama mtandao uliobora kati ya sisi nayeye tunapofanya kazi ya Mungu.Na hii mifano alitoa katika eneo tofauti na shughuli tofauti hadi wanafunzi kumwomba awaongezee lmani.
Tusome Matayo 17:20
« Kwa sababu ya imani yenu haba. Nawambieni hata kama tu mkiwa na imani , iwe ndogo hata kama mbegu ya haradali mtaweza kuuambia mlima huu:Toka hapa uende pale ,nao utakwenda. Hakuna chochote ambacho hakitawezekana kwenu. »
-Hili lilikuwa ni eneo moja Yesu aliwafunza mitume kuhusu imani. Ukisoma Matayo 17:14-16 utoana mtu mmoja akimlilia Yesu amwonee huruma maana mtoto wake alikuwa na kifafa.
Mtu huyu akamwambia kuwa wanafunzi wake wameshindwa kumfukuza huyo pepo.
Ndipo Yesu akamkemea akatoka. Mitume walimwendea Yesu na kumuuliza sababu wao wameshindwa. Naye akawajibu kuwa imani yao ndogo.
Ukisoma matayo 17:17 Yesu anajaribu kuwaeleza kwamba hatakuwa na wao kila siku ndiyo wamletee kilichoshindikana ,ila kinachostahili au kinachohitajikana kwao ni mtandao bora(lmani). Sema amina!
Ndiyo maana nakwambia si lazima unayemwombea awe na imani . wewe mwenye kuomba ukiwa na imani atapona.Ukiwa na imani hakuna pepo litakalosimama mbele yako ,shida utafukuza ,Halleluya!
-Eneo la pili: Matyo 21:21-22
» Yesu akamjibu ,Kweli nawambieni kama mkiwa na imani bila kuwa na mashaka ,mnaweza kufanya hivyo ,bali hata mkiuambia mlima huu:Ng’oka ukajitose baharini itafanyika hivyo.
22. Na mkiwa na imani chochote mtakachoomba kwa sala mtapata. »
Ukisoma Matayo 21:19-20 utaona Yesu akipita akauona mti usiye na matunda akaulaani maana alikuwa na njaa.
Baada tu ya kupita wanafunzi wake wakastajabishwa na kuuona ukikauka ghafla. Walimuuliza akawajibu kwamba ukiwa na imani waweza chochote.Halleluya!
Nataka uchuke tabia mpya leo,yale yanayokusumbuwa kimaisha,yale yamevunja moyo wako,hizo shida hata kwetu katika familia simama ulaani hayo ukiwa na imana. Anza kunena mazuri,mema kwa familia,kwa nchi ,kwa kanisa la Mungu maana ukiwa na imani utabadirisha hali.
-Eneo la tatu : Tusome Luka 17:6
« Naye Bwana akajibu ; Kama imani yenu ingekuwa ndogo hata kama chembe ndogo ya haradali ,mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu : Ng’oka akajipandikize baharini ,no ungewatii. »
Kutoka Luka 17:3-5 utasoma uone vile mitume aliwafunza kusamehe. Ndugu yako akikukosea arudi atubu hata mara saba msamehe. Aliwafunza kwamba bila imani huwezi samehe mtu. Ukiwa na imani una mamlaka,una nguvu ya kimungu ya kutenda chochote kadri ya mapenzi yake Mungu. Unaweza hata epuka dhambi ukitumia imani sio kuwa kila siku unajihurumia ,Eee Mchungaji niombee nimeanguka tena katika dhambi. Kataa dhambi katika imani.
Ushuhuda: Nakumbuka tukiwa gerezani tumeomba na Mungu akatufunulia kwamba tutatoka ila tufanye maombi ya siku 3 tukifunga.
Baadae hakimu alituma mtu akasema ,nitafutieni laki mbili niwatoe maana kesi zenu ni tupu.
Tulisimama na kuomba tukimwambia Mungu,Bwana wa majeshi mwenye haki ni wewe uliahidi. Pesa hatuna na hata tungekuwa nazo hatutaki kufanya dhambi ya kupatiana hongo/rushwa/ufisadi.
Kulingana na imani hiyo Mungu alitutoa bila hata kulipa chochote maana ameona imani yetu ulikuwa bila mashaka. Halleluya!
Kwa ufupi tunaweza kuwa na picha ifuatayo:
√Huwezi samehe bila imani; Luka 17:3-6.
√Huwezi fukuza mapepo,hali ngumu za kimaisha,nkt bila imani. Matayo 17:17-20.
√Huwezi jibiwa maombi kuhusu chochote bila imani. Matayo 21:21-22.
Ubarikiwe ndugu dada msomaji kwa kutufuata ,mtii neno hili. Amina!