Bwana Yesu Kristo aliye Mfalme na Mwokozi wetu asifiwe sana!
Naitwa Mchungaji Uwisezerano Libéré ninawasalimia sana katika jina la Yesu Popote mlipo.
Neno ningependa tuchangie leo lina kichwa kisemacho : AHADI
________
Tusome kitabu cha Hesabu sura ya 23:19-20.
« 19 Mungu si mtu aseme uongo wala si binadamu abadili nia yake! Je ,ataahidi kitu na asikifanye au kusema kitu asikitimize?
20 Tazama nimepewa amri ya kubariki naye amebariki wala siwezi kuitanguwa.
Bwana asifiwe sana! Ningependa leo ufunuliwe zaidi kuhusu ahadi yake Mungu kwa maana si ahadi ya binadamu ambaye anaweza kukuahidi kukutendea hili na lile mwisho we akashindwa kutimiza. Kutoka hapo utakuwa na picha mpya ili uweze kumtumainia Bwana tena.
Wengi mnajua sana hadisi hii kuhusu Balaki akiwa adui wa wana lsraeli akaleta Balamu amlaaniye taifa teule hili maana kila mtu alikuwa anawaogopa; badala Balamu kuwalaani akawabariki kwa maana huwezi laani wateule wa Mungu ,huwezi laani waliobarikiwa na Mungu.
Soma Hesabu 23:8.
Nataka nikwambie wewe umesubiri kwa muda mrefu ahadi yoyote ile na wewe umesubiri kwa umakini Ahadi Mungu alitolea wanaburundi. Labda uko ukimbizini kwa kambi ukiwa Tanzaniya,Rwanda,Uganda,Afrika ya kusini,Zambia ,Malawi na popote pale mwanaburundi ulipo kwa ajili ya shida zilizotokea nchini mwetu; Usinung’unike hata kidogo.
Mungu si mtu abadili nia yake,alisha sikia kilio chako akasema nakuja haraka kuitimiza ahadi yangu kuhusu taifa langu teule la Burundi na si kesho wala kesho kutwa.
Tazama kuna fununu kutoka kote duniani kwamba matatizo ya Burundi amekosa suruhu. Hiyo ndio ilikuwa ishara Mungu alitoa kwa wamchao ya kwamba mgogoro wa Burundi utakosa mtatuzi ,mataifa atakaa,Umoja wa mataifa,Umoja wa ulaya na wale wengine wote wamekuwa wakikandamiza wateule wangu lakini hawatapata suruhu.
Na papo hapo ndipo Mimi mwenyewe Mungu aliyeziumba mbingu na nchi nitasimama nijitukuze niabishe mataifa na ufalme wa ashuri. Watu wangu wamekuwa wakiteswa na shetani akitumia ukabila,vyama vya siasa ,ubguzi wa aina yote na mikoa nakadharika.
Ndugu ,dada unasoma ujumbe huyu popote ulipo tazama Mungu amekwisha simama ,jitakase maana atembeae na Mungu si muovu wala mtenda dhambi. Muda sio mrefu tubu leo ,ikiwa ulijisahau ukajichanaganya na mambo ya wasiomjua Mungu au kama umetembea katika tabia za mataifa mengine omba msamaha Mungu ni mwaminifu maana atakaye ingia nchi mpya ya Burundi kesho kutwa ni yule ambaye damu yake Yesu iko juu yake. Kwa sababu malaika akitumwa leo kuangamiza farao na nyumba yake na watu wake wewe hautakufa.
Gidiyoni Malaika akamtokea,akamkuta mahali pa uficho akamwambia » Bwana Yu pamoja nawe Eee shujaa » soma kitabu cha Waamuzi 6:12 na akamwambia tena « Amani iwe pamaoja na wewe ,usiogope hautakufa. » soma Waamuzi 6:23.
Bwana anakuja akupatie amani Eee shujaa wewe ulisubiri muda mrefu,utarudi nchini ukilitukuza jina lake Mungu. Na wewe uko bado nchini nakutia moyo endelea kumwomba Mungu na kunyenyekea mbele zake utalindwa hautakufa.
Burundi ni taifa Mungu alikusudia amani ,maendeleo na kupeleka uvuvio wa injili kwa ngazi ya kimataifa maana mataifa hayo yamemuasi Mungu. Ni vizuri msomaji ujuwe kwamba kabla Yesu Kristo arudi kulichukuwa kanisa ni lazima injili njema ihubiriwe duniani kote iwe ishara kwa mataifa ya kwamba Masihi yu karibu sana na utaanzia Burundi.
Katika kitabu cha Kutoka 14:14″ Musa akawambia wana lsraeli Bwana atawapigania ninyi mtanyamanza kimya » akawapasulia njia katika bahari ya shamu wakavuka salama.
Leo Mungu atawapigania Ee nyi wanaburundi mtakumbuka yaliowapata kama historia tu .
Ashukuriwe Bwana wa majeshi kwa kuwa hata ukihangalia na macho ya kawaida unaweza ona kwamba amekwisha anza kazi ya ukombozi wa taifa lenu.
Msomji wetu leo nakomea hapa tutashirikiana tena kesho nizidi kukumbusha ahadi zako!
Bwana Yesu Kristo akulinde na akutetee unapo litii neno lake na kutubu,ubarikiwe sana !