Bwana Yesu asifiwe ! Ninamshukuru Mungu kuturehemu na kutupatia siku hiyi ili tufurahie upendo wake.
Baba uishiye milele nakuhimidi umeinuliwa juu ,umetukuka. Naomba mapenzi yako afanyike duniani kama alivyo mbinguni katika jina la Yesu Kristo.
Amen!
Msomaji tulikuahidia kuendelea na mada hii ya lmani. Leo ni lmani lll.
Tusome Efeso 6:16
« Zaidi ya yote lmani iwe daima kama ngao mikononi mwenu iwawezeshe kuzima mishale ya moto ya yule mwovu. »
Halleluya!
Paulo akiwandikia cheti hiki waefeso ,aliwapatia picha ya mwanajeshi au askari mkristo vile anapaswa kuwa ili amshinde shetani.Ndiyo akamwambia basi ,kwa sababu hiyo chukuweni silaha zote za Mungu ili siku ile itakapofika mweze kuyapinga mashambulio ya adui. Efeso 6:13.
Sasa kutoka hapo aliorodhesha silaha zote na lmani ikapata nafasi ya 4. Inaitwa tena ngao.ukiwa na imani unama mishale ya ibilisi ,hata maisha awe magumu aje hautapotoka ,maana majaribu anakuwa ya muda tu.
Ukitumia imani we ni mshindi ,we shujaa .Ningependa leo tuangalie waliotutangulia kuwa mashujaa wa imani katika bibliya.Walikuwa watu na utu kama sisi. Je ,kama waliweza si nasisi tunaweza ?
1)Abeli kwa imani alimtolea Mungu sadaka ikampendeza Mungu kuliko ike yake kaini . Unapotoa sadaka yako ndugu ,uwe na imani bila hiyo haitakubalika.
2) Henoki kulingana na kiwango chake cha imani Mungu alimchukua bila kufa au kuhonja mauti.
3) Noa(Nuhu) ,kwa imani alitii Mungu akajenga safina.Mwenye imani hawezi kuwa mjeuli bali humtii Mungu.
4) Abrahamu ,kwa imani alitii alipoitwa ,akaenda bila kujua aendako bali kamtegemea Mungu pekee.
5) Kwa imani Sara ,tasa kabisa alipata mtoto Samuel. Aliamini kwamba Mungu hutimiza ahadi yake. Akapata mimba akiwa mzee. Nkwambia ukiwa na imani haijalishi we una umri gani ,mambo yote yawezekana.
6) Kwa imani lsaka aliwabariki Yakobo na Essau. Yakobo akaja kubadirishwa jina akaitwa lsraeli.
7) Yakobo ,kwa imani alibariki wanawe ,akamwabudu Mungu.
8) Kwa imani ,Mose alifichwa na wazazi wake kando ya mto Nili. Hawakuiogopa amri ya farao .
10. Kwa imani Mose alikataa kuitwa mtoto wa binti ye Farao.Aliona ni heri kuteseka pamoja na watu wa Mungu kuliko kufurahia dhambi. Alirudi pia kumwambia farao aachilie wanaisraeli waende kumwabudu Mungu hakuogopa kuuawa maana alikuwa ameondoka misri baada ya kumuua mumisri akiwa anatesa wanaisraeli.
Ndugu ,dada tuendelee kesho kuwaona mashujaa wa imani katika bibliya. Soma cha Waebrania 11:4-27, ujisomee yale nilikuwa nakusimulia hapo juu.
Mbarikiwe sana ,mnapoamini Mungu zaidi katika Kristo! Amina!