Imani (4)

Bwana wa majeshi ,Bwana wa mabwana ashukuriwe tumeona siku nyingine mpya. Mwezi Mungu tunanyenyekea mioyoni mwetu ututumie vile upendavyo ,utuoshe tutakasike na mapenzi yako afanyike katika jina la Yesu Kristo, Amina!

Mchungaji Uwisezerano Libéré ndiye mko pamoja.

Basi leo ningependa tumalizie mada yetu Kuhusu lmani :Imani IV.

Tusome Waebrania 12:2

« Tumwelekee Yesu ambaye ndiye alianzisha imani yetu na ambaye ataikamilisha. Kwa ajili ya furaha iliyokuwa inamngojea yeye alivumilia kifo msalabani bila kuijali aibu yake na sasa ameketi upande wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu . » Halleluya!

Bwana asifiwe sana! Ikiwa ni Mungu alianzisha imani ndani yetu ni yeye kuikamilisha.lmani yetu kama wanaburundi ni kabla twende Mbinguni taifa letu litakuwa na amani ,uvuvio wa injili,maendeleo na Mungu atatutumia kwa njia ya ajabu wanaburundi hawatazozana tena kuhusu kabila,vyama au chochote kile. Taifa letu litakuwa kielelezo. Na mambo kama haya shetani siye mwanzilishi,hapana bali ni Mungu mwenyewe. Nataka leo umwamini Mungu maana ,wewe usiye na imani unatuchelewesha kutua katika ile ahadi. Kitu kingine ,neno limezungumzia ni kuwa Yesu furaha yake nikuona imani yetu ikikamilishwa na kuona kuona ahadi yetu ikikamilishwa pia maana hizi shida zote yeye yazijua vyema. Hawa viongozi wa wa dunia hiyi wakatili naye walimweka msalabani wakamuua japo ilikuwa ndiyo njia yetu kukombolewa. Ndiyo sababu alishapaka mafuta mteule wake wa kuiongoza Burundi katika ahadi yake ,halleluya!

Tuendelee kuangalia walemashujaa wa imani kama nilivyowaahidia. Na leo inafaa hata wexe uingine kwenye orodha ya mashujaa.

(Kutokana na orodha nilikuwa nayo jana hadi 10 ,leo nitaanzia 11).

11.) Kwa imani Mose aliadhimisha siku ya pasaka ,akaamuru damu inyunyiziwe juu ya milango ili malaika muangamizi asiwaue wazaliwa wa kwanza wa lsraeli.

12) Kwa imani Waisraeli walivuka bahari ya shamu lakini wale wamisri waliowafuata hawakukuwa na imani walifia baharini. 

13) Kwa imani kuta za yeriko zilianguka baada ya waisraeli kuzunguka siku saba.

14) Kwa imani Rahabu yule malaya mkubwa mnayemjua kwa sababu za kuficha na kuwakarbisha wapelelezi waisraeli aliokoka. Ukisoma kitabu cha Mathayo 1:5 utamkuta ako kwenye orodha ya mababu wa Yesu Kristo. Usishangae.

Waebrania 11:32-33 

« 32. Basi niseme nini juu ya Gideoni ,Baraki,Samsoni ,Yefta ,Daudi ,Samueli na Manabii.

33. Kwa imani walipigana vita wakashinda. Walitenda mambo adili ,wakapokea yale alioahidi Mungu. Walifunga vinywa vya simba. » Halleluya!

Msomaji wetu nataka kuanzia leo ujue haya mambo vizuri usije ukakaa tu unasubiria. Mungu atakuwezesha kukufanikisha kutenda maajabu kuhusu ahadi yake ukiwa na imani. Hili ni ukweli. Sasa (1) ahadi ipo. (2) imani yako inasababisha ahadi yako/yetu kwa taifa letu ikamilike ; (3) matendo yako kuhusu ahadi ndiyo atafunguwa njia ili uweze kuingia.

Mfano tu kidogo: Mungu aliahidi kwamba atatoa mwanawe ili mwanadamu akombolewe. Yesu alikuja akafundisha watu njia ya ukweli lakini viongozi wa dini na serikari za kiroma walimkataa,mafarisayo walimkataa. Je,unafikiri wangekosa ujasiri wa kumuua Yesu wewe ungekombolewa? Ndiyo maana aliwasamehe maana walifanya kazi yao ya kumuua ndiyo ahadi na maandiko ya manabii vitimike. Leo sasa simama ,omba ,uliza Mungu ufanye nini ndiyo ahadi itimie.

Msomaji wetu mpendwa tunakomea hapa kuhusu mada hiyi leo,nakuombea Mungu akutie nguvu ,imani yako iimarishwe na uanze kutenda kulingana na imani hiyo kuhusu ahadi katika jina la Yesu Kristo.amina!