Mwenyezi- Mungu apewe sifa na utukufu ,Jehova Rapha anayetuponya kila siku,amina!Tuombe: Baba mwenye mamlaka yote duniani hata mbinguni,tunakushukuru maana matendo yako ni makuu. Uendelee Baba kujidhihilisha katika watu wako katika jina la Yesu Kristo.
Mchungaji Uwisezerano Libéré,nawasalimu katika jina la Yesu Kristo !
Leo tunaanza ukurasa mpya yaani mada mpya.
Lengo la madi hiyi ni ;TURUDISHE WATU KUMWOGOPA NA KUMCHA MUNGU.
Tusome Zaburi 111:10
« Kumcha Mungu ni msingi wa hekima ; wote wanaozitii amri zake hujaliwa busara. Sifa zake zadumu milele . »
Tusome tena Danieli 6:26-27.
« Nitatoa amri kwamba watu wote katika ufalme wangu ni lazima wamwogope na kumcha Mungu wa Danieli. Yeye ni Mungu aliyehai ,aishiye milele : Ufalme wake kamwr hauwezi kuangamizwa ,utawala wake hauna mwisho.
Yeye hukomboa na huokoa ,hufanya ishara na maajabu mbinguni na duniani maana ameokoa Danieli makuchani mwa simba. »
Hayo ni maneno na amri vilitolewa na mfalme Dariyo baada ya Danieli kutupwa katika pango lile la simba na kumkuta bado ako hai, simba hawakumdhuru.
Daudi naye akasema kumcha Mungu ni msingi wa hekima ,mtiifu wake Mungu hujaliwa busara.
Watu wa siku hizi hawana ile hali ya kumwogopa Mungu ,hawamchi Mungu ndiyo maana dunia na tabia za watu zilisha haribika ,watu wanaishi kwa maovu wamesahau yakwamba Mungu anaweza kuokoa ,kukomboa maana uweza wake niwa ajaabu mno. Kama wewe hauna hekima kutoka mbinguni jua kwamba uko katika shida ulimwenguni.
Aliyepata kujua ni Mfalme Farao wa Misri ambaye aliwazuilia wanaisraeli utumwani nchi mwake na kupata mapigokali ya Mungu hadi kumi na moyo wake bado ukasalia kuwa mugumu. Tuangazie vizuri mapigo hayo moja kwa moja ndiyo tuelewe Mungu niwa ajaabu usijiachie katika mambo ya kihuni ya dunia hiyi:
1) Kutoka 7:14-25.
Maji kote aligeuzwa kuwa damu. Samaki walikuwamo mtoni Nili walikufa ,nchi nzim ikanuka vibaya wamisri wakachukia kunywa maji.
2) Pigo hili tunalikuta Kutoka 8:1-15 ambapo Mungu alijaza vyura hadi kumpandia Farao. Wachawi wake nao walileta vyura lakini wahakuweza kuviondoa .
3) Pigo la tatu liko Kutoka 8:16-19.
Mungu alipiga Misri na chawa au viroboto. Chawa walipandia watu na vitu ,wachawi wake Farao hawakuweza kuleta chawa wengine ndiyo mstari wa 19 wakamwambia mfalme ya kwamba jambo hilo lilikuwa ni chanda(kidole) chake Mungu.
4)Pigo la nne Kutoka 8:20-32.
Walipigwa na makundi ya nzi. Nzi waliwatesa Farao na watu wake wakaribu na nchi nzima. Lakini cha kushangaza haya mapigo hayakugusa sehemu za #Gosheni mahali ambapo waisraeli walikuwa wanaketi.
5) Pigo la tano ni Kutoka 9:1-7.
Hili lilihusu maradhi mabaya juu ya mifugo ,farasi,ngamia ,punda nkt.
Lakini mifugo ya wanaisraeli haikuguswa hata kidogo. Halleluya!
Ndugu ,dada mogope Mungu,muche MUNGU niwa ajabu. Kidole chake hutenda maajabu. Leo tukomee hapa tutaendelea kesho kwa mapenzi yake Mungu! Ubarikiwe sana!