Ugopeni Mungu wetu.

Mungu Bwana wa majeshi apewe sifa na utukufu maana ametufikisha siku hiyi.Ndugu dada msomaje wetu mpendwa nakusalimu katika jina la Yesu Kristo!

Kama ilivyo,tuendelee na mada yetu:TURUDISHE WATU KUMWOGOPA NA KUMCHA MUNGU.

Ningependa leo tuendelee kuangazia mapigo tano yaliobaki katika yale 10 Farao na wamisri walipigwa na Mungu.

6) Pigo hili tunalikuta Kutoka 9:8-12.

Pigo hili likikuwa majipu ambayo alileta vidonda kwa watu na wanyama kila mahali nchini Msri.

7) Pigo hili Kutoka 9:13-35.

Pigo hili lilihusu mvua ya mawe na ngurumo ilipiga nchi yote. Watu na mifugo vilivyobaki vikaangamia. Mashamba, miti,mimea, vyote vikafa.

8) Pigo la nane hili,twalisoma Kusoma 10:1-20. Nzige walivamia nchi na kula chochote kilichobaki wakati wa mvua ya mawe.

Kutoka 10:1-2

 » Mwenyezi Mungu akamwambia Mose nenda kwa Farao ,mimi nitamfanya kuwa mkaidi na maofisa wake ili nipate kutenda ishara hizi miongoni mwao. Ili nyinyi mpate kuwasimulia watoto wenu na wajukuu wenu jinsi nilivyowadhihaki wamisri kwa kuzifanya ishara hizo miongoni mwao. Hivyo mtatambua kuwa mimi ndimi Mwenyezi Mungu.

9) Pigo la tisa liko Kutoka 10:21-29. Pigo hili lilikuwa la giza. Watu hawakuweza kuona au kuondoka kwa muda wa siku 3.

Lakini haya yote hayakupa sehemu ya Gosheni pale waisraeli waisraeli walikuwa wameketi ,mwangaza ulikuweko.

10) Pigo la kumi na ni lamwisho tunalikuta Kutoka 12:29-36. Lilikuwa kifo kwa wazaliwa wote wa kwanza nchini Misri kuanzia kwake Farao hadi mifugo. Ikawa ni huzuni ma kilio maana tukio kama hili halijawahi onekana duniani tena.Kama Mkristo au yeyote unayesoma leo,ujue unapomwasi Mungu unapokataa kumcha na kumwogopa Mungu,unaleta shida ndani ya nyumba yako ,katika familia ,kwa majirani wako,katika kanisa,nchini mwako hata duniani.

Swali hapa: Watoto wachanga walikuwa hawana dhambi au hatia wanyama na mazingira yote yalikuwamo katika ile miji miwili ya Sodoma na Gomora ; Kwa nini hao watoto waliangamia? Kwa nini vitu hivo viliangamia pia?

Si kwa ajili ya dhambi za watu wazima ? Au wale watu maskini walikuwamo Misri wakati huyu Farao ,ambao unakuta hata hawakufaidika chochote au hawakuhusika na mateka ya waisraeli ,kwa walifisha wana na mifugo ? Si kwa ajili ya dhambi za viongozi nchini?

Ndiyo sababu nawauliza wanaburundi na wale mnasoma ,acheni dhambi ,mche Mungu.

Kama tusomavyo Kutoka 12:21-23,

Waisraeli Mose aliwaagiza kumchinja mwanakondoo na kunyunyiza damu yake kizingitini cha juu na miimo miwili ya mlango. Na Yeyote asitoke mlangoni mwa nyumba ili malaika ikija kuangamiza asiwauwe wazaliwa wa kwanza katika lsraeli.

Mwanakondoo huyu,hulinganishwa na Yesu Kristo. Hivi ndivyo itakuwa nchini mwetu kwa wale ambao juu yao damu yake Yesu haitaonekana. Atakufa maana ni lazima Mungu akomboe watu wake na malaika ataangamiza kila mwovu ,Burundi mpya wataiona watakatifu na waliooshwa na damu ya Yesu pekee.

Ndugu dada mpendwa ,nakutakia kuoshwa na damu ya Yesu leo ndiyo uweze kuiona ahadi. Tukutane tena kesho kwa majaliwa ya Mungu . ubarikiwe unapoqmini Mungu!