SABABU ZINAZOFANYA MAOMBI  YAKO YAKOSE MAJIBU.

1. KUTOKUJUA KUOMBA IPASAVYO

Hii ni sababu inaweza kuyafanya maombi yako yasipate kibali

1 Ikawa alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, Bwana, tufundishe sisi kusali, kama vile Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake.

Luka 11 :1

Hapa  tunaona kutojua kuomba kunatufanya kuwa na mawasiliano dhahiri mbele za Bwana.

3 Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu. 

Yakobo 4 :3

54 Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya]? 

Luka 9 :54

55 Akawageukia, akawakanya. [Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.] 

Luka 9 :55

56 Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine. 

Luka 9 :56

Hatakuomba ili wengine waangamie ni kutokujua kuomba pia…

16 Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni; na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona. 

Yohana 16 :16

Yesu amekuita uwaombee wanaopotea na kuziacha njia za Bwana. Hakikisha unaombea wengine mema ili ujibiwe Maombi yako .

Roho Mtakatifu naye anaujua udhaifu wetu kwamba hatujui kuomba ipasavyo .

26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. 

Warumi 8 :26

27 Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu. 

Warumi 8 :27

Hivyo tunapaswa kumwambia Roho Mtakatifu atufundishe kuomba ili kuomba kwetu kuwe na majibu

2. KUKOSA UTII MBELE ZA MUNGU

9 Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria, Hata sala yake ni chukizo. 

Mithali 28 :9

Kutokutii maagizo ya Mungu na kugeukia njia mbaya hunazuia kuomba kwetu kusiwe na majibu wala Mungu hawezi kusikia maombi Yetu .

14 ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao. 

2 Mambo ya Nyakati 7 :14

Kwahyo kutokutii sheria za Mungu kunazuia Mungu asijibu maombi yetu .

1 Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. 

Zaburi 1 :1

2 Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku. 

Zaburi 1 :2

3 Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa. 

Zaburi 1 :3

Maombi yako yanategemea uhusiano mzuri na Mungu kwa kufuata maagizo .

8 Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana. 

Yoshua 1 :8

3. KUTOKUZAA MATUNDA:

Kutozaa matunda ni kutokuwa na matokeo mazuri mbele za Mungu .

9 Kama vile Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo langu. 

Yohana 15 :9

10 Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake. 

Yohana 15 :10

11 Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe. 

Yohana 15 :11

12 Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi. 

Yohana 15 :12

13 Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. 

Yohana 15 :13

14 Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo. 

Yohana 15 :14

15 Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu. 

Yohana 15 :15

16 Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni. 

Yohana 15 :16

17 Haya nawaamuru ninyi, mpate kupendana. 

Yohana 15 :17

10 Na shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni. 

Mathayo 3 :10

Unaweza ukawa umejaa neno la Mungu kwa wingi sana lakini kama huleti matokeo mazuri au hulitendei kazi neno na kuleta matokeo katika maisha yako maombi yako yatakosa majibu huko ni kutokuzaa matunda .

9 Na sasa hivi shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni. 

Luka 3 :9

MUNGU AKUBARIKI SANA

Publicités